Klabu ya soka ya Simba inakabiliwa na ratiba ngumu ya michezo yake ya ligi kuu pamoja na ile ya kimatafa ambapo mara baada ya michuano ya Sportpesa Super Cup inayoanza 22/01/2018 hadi 27/01/2019 timu hiyo itaondoka kwenda Misri kwa ajili ya kukipiga na Al Ahly.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Februari 2, 2019 saa 3 usiku kwa saa za Misri na saa 4 usiku kwa saa za Tanzania na baada ya mechi hiyo Simba itarejea nchini kucheza na Mwadui FC Februari 6, 2019 kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam.
Baada ya mchezo dhidi ya Mwadui Simba itajiandaa na mchezo wa marudiano na Al Ahly utakaopigwa jijini Dar es salaam Februari 12, 2019 10:00 jioni.
Baada ya mchezo dhidi ya Al Ahly Simba itakuwa na siku 4 za kujiandaa na mchezo dhidi ya Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara timu ya Yanga mchezo ambao utapigwa Februari 16, 2019 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Ratiba ya mechi zingine.
19/02/2019
Africa Lyon Vs Simba - Dsm
22/02/2019
Azam Vs Simba - Dsm
26/02/2019
Lipuli vs Simba - Iringa
03/03/2019
Stand United Vs Simba - Shinyanga
Baada ya hapo Simba itarejea Dar es salaam kujiandaa na michezo ya klabu bingwa Afrika ambapo Machi 9, 2019 itakuwa ugenini kucheza na JS Saoura utakaopigwa saa 2:00 usiku kwa saa za Algeria na saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania.
Kisha itacheza mchezo wa misho kwenye makundi ambao utapigwa jijini Dar es salaam Machi 16, 2019 dhidi ya AS Vita Club kwenye uwanja wa taifa. Kisha itamaliza mwezi Machi kwa kucheza mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting na Mbao FC ambazo zote zitapigwa Dar es salaam.