Kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji aliyekuwa anaichezea Tottehan Hotspurs ya England Mousa Dembele, leo ameripotiwa kuihama rasmi club hiyo na kujiunga na Guangzhou Evergrande ya China kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mousa Dembele mwenye umri wa miaka 31 anajiunga na club hiyo kwa ada ya uhamisho inayotajwa kufikia pound milioni 11, Dembele anaondoka Tottenham baada ya kudumu na timu hiyo kwa miaka 7 toka alipojiunga nayo mwaka 2012 akitokea Fullham kwa uhamisho wa pound milioni 15.
Hata hivyo sababu ya Dembele kwenda kucheza China inatajwa ni kutokana na kuwa na majeruhi ya muda mrefu, akiwa hajaingia uwanjani toka November 3, hivyo aliamua kuondoka EPL kutokana na Ligi hiyo kuwa na mikiki kutokana na kukumbwa na majeraha asingeweza kuhimili heka heka za EPL.
Dembele ambaye amekuwa nje kutokana na kuwa na jeraha la kifundo cha mguu iliyomplekea kukosa michezo 18 ya Tottenham msimu huu, alikuwa amebakiza mkataba wa miezi sita wa kuitumikia Tottenham, ambapo ungemalizika mwisho wa msimu huu.
“Anafikisha umri wa miaka 32 wakati wa majira ya joto na amekuwa na mfululizo wa majeraha katika misimu nane iliyopita na tayari amekiri kuwa mwili wake hauwezi kuendana na mikikimikiki ya EPL, alikuwa anataka kwenda katika Ligi yenye uhitaji mdogo (phyisical)” aliandika mwandishi wa Ubelgiji