Mwishoni mwa mwaka jana msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael Lulu alivishwa pete ya uchumba na Mkurugenzi Mtendaji wa E FM/E TV, Francis Anthony Ciza a.k.a Majay.
Hivi karibuni Lulu akigawa nguo kwa mashabiki wake ambao walijitolea kununua, alionekana akiwa
hana pete ya uchumba kidoleni kitu ambacho kilibua mjadala.
Mazungumzo hayo yalifika mbali zaidi na wengine kueleza kuwa mrembo huyo siku chache zilizokuwa zimepita alipokea kipigo kutoka mchumba wake.
Hata hivyo wawili walionekana kutupilia mbali tetesi hizo zilizokuwa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.
Leo mapema kwenye kipindi cha Joto la Asubuhi kinachoruka E FM, Lulu ameonekana akiwa amevaa pekee yake kidoleni kitu ambacho kinachokuja kumaliza uvumi wote uliokuwa ukienea. Je, ni kwanini pete ya lulu imeteka mazungumzo?.