MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Faidha Omari ‘Sister Fay’ ametaja sababu ya kuacha kumposti mume wake Elias Njau akidai kuwa jamaa huyo ndiyo chanzo cha yeye kukamatwa na kuwekwa lumande.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda Sister Fay alisema kuwa bado yupo na baby wake huyo lakini hamposti tena kwa kuwa alikamatwa kwa sababu yake kutokana na maneno ya watu kwamba anambemenda kwani ni mdogo kwake kiumri.
“Nipo na mume wangu kama kawaida lakini siwezi kumposti kwa sababu nilikamatwa kwa sababu yake ingawa tulipofika polisi wakakuta umri wake unaruhusu, si mdogo kama walivyodhani, huyu nitaishi naye milele mpaka kifo kitute-nganishe ila kwa mitandao sasa anapu-mzika, ”alisema Sister Fay.
Hii Hapa Sababu ya Sister Fey Kutompost Mpenzi Wake
0
January 28, 2019
Tags