Uongozi wa Yanga umeweka wazi kikosi kinachosafiri hii leo kuelekea visiwani Zanzibar kwaajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Michuano hiyo hufanyika kila mwanzoni mwa mwaka kuanzia Januari mosi hadi kilele cha sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12.
Kikosi cha wachezaji 23 cha Yanga kinachosafiri hii leo kuelekea visiwani humo ni: Maka Edward, Haji Mwinyi, Said Makapu, Matheo Anthony, Erick Msagati, Deo Mkami, Ibrahim Abrahaman, Ibrahim Ahmed, Deus Kaseke, Mustapha Seleman, Abuu Shaban, Ramadhan Mrisho.
Wengine ni: Mohamed Salumu, Cheda Hussein, Yasini Salehe, Salumu Mkama, Faraji Kilaza, Bakari Athman, Said Khasimu, Shaban Mohamed, Pius Buswita, Juma Abdul na Jaffary Mohamed.
Awali kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alitangaza kuwa nyota wengi wa klabu hiyo hawatosafiri na timu katika michuano hiyo kutokana na sababu kadhaa zikiwemo majeraha na kupewa mapumziko mafupi.
Michuano hiyo ilianza Januari mosi kwa mchezo mmoja kupigwa ambapo KVZ SC walitoa sare ya bila kufungana na Malindi SC, na leo ratiba ya michuano hiyo itaendelea kwa michezo miwili kupigwa ambapo mchezo wa kwanza wa saa 10:00 jioni, Chipukizi wataikaribisha Mlandege na mchezo wa saa 2:00 usiku, Azam FC itawakaribisha Jamhuri SC. Mechi zote zitapigwa katika uwanja wa Amaan.
Hiki Hapa Kikosi Cha Yanga Kinachokwenda Mapinduzi CUP
0
January 02, 2019
Tags