Wakati Dunia ikishuhudia mjadala mkubwa hivi sasa juu ya ubora wa nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi na gwiji wa soka Diego Maradona, mwenyewe ameuzungumzia kwa namna ya tofauti.
Messi ambaye ni mshindi mara 5 wa tuzo ya Ballon d'Or amesema kuwa anapata ukosoaji mkubwa hata kwa watoto wake hasa mwanaye mkubwa, Thiago.
"Anafahamu sana kuhusu soka kwasababu ni mkubwa , na anazungumzia sana vitu vingi ambavyo vinafanyika katika soka", amesema Messi.
"Nimekuwa nikipata ukosoaji mkubwa kutoka kwake, anafuatilia Barcelona, La Liga, Klabu Bingwa Ulaya na anapenda. Anauliza maswali na huwa ananipa muongozo pale mambo yanapokuwa mabaya, huwa ananilazimisha nimuelezee kwanini hatushindi na hapo huwa tunaongea mambo mengi", ameongeza Messi.
Hivi karibuni Messi amefikisha idadi ya mabao 400 ya La Liga, katika mchezo dhidi ya Eibar ambao umemfanya kuendeleza rekodi yake ya ufungaji bora wa muda wote wa ligi hiyo.
Mjadala wa ubora wa Messi dhidi ya Maradona umeshika kasi huku magwiji kadhaa wakitoa maoni yao ambapo kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ameungana na gwiji wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Scotland, Graeme Souness akisema kwamba Messi ni mchezaji aliyedumu katika ubora kwa muda mrefu tofauti na Maradona.