Idadi ya Waliofariki Katika Shambulio Kenya Yaongezeka Yafikia 21

Idadi ya Waliofariki Katika Shambulio Kenya Yaongezeka Yafikia 21
Idadi ya watu waliofariki katika shambulio la wanamgambo wa Somalia, walipoivamia hoteli moja mjini Nairobi imeongezeka hadi 21 kwa mujibu wa serikali.

Mamia ya watu walilazimika kutoroka umwagikaji damu ulioshuhudiwa katika hoteli ya DusitD2 na jengo la kibiashara siku ya Jumanne.

Watu 28 waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali, huku wengine 19 wakiwa hawajulikani waliko, shirika la msalaba mwekundu linasema.

Kundi lililoko nchini Somalia al-Shabab limekiri kuhusika na shambulio hilo, lililozusha operesheni ya saa 19 ya kiusalama.
Rais Uhuru Kenyatta Jana Jumatano alitangaza kwamba washambuliaji hao wameangamizwa na kwamba operesheni ya uokozi imekamilika.

Kenya imekuwa ikilengwa na kundi la al Shabab tangu Okotoba 2011, wakati taifa hilo lilipotuma vikosi vyake nchini Somalia kupambana na kundi hilo la jihadi.

Miongoni mwa wahanga wa shambulio hilo ni pamoja na mmoja aliyeponea shambulio la kigaidi la 9/11 , Shabiki sugu wa soka, na marafiki wawili wa dhati.

Feisal Ahmed, mwenye umri wa miaka 31, na Abdalla Dahir, wa miaka 33, washauri waliofanya na kampuni ya kimataifa Adam Smith International (ASI), walikuwa wakila chakula cha mchana pamoja katika mgahawa wa Secret Garden uliopo katika sehemu ya chini ya hoteli hiyo wakati mlipuaji wa kujitoa muhanga alipojilipua.


"Walikuwa na uhusiano wa karibu sana," Shemegi yake Ahmed Abdullahi Keinan ameliambia shirika la habari la Reuters.

"Walikuwa na uhusiano wa karibu sana kiasi cha watu hata kusema watakufa pamoja."

Abdalla Dahir (kushoto) na Feisal Ahmed (kulia) wanasemekana kuwa na ukaribu sana
Walikuwa wakifanya kazi katika wakfu wa ustawi wa Somalia uliosimamiwa na ASI "kuleta amani na ustawi kwa nchi ya Somalia", ASI imesema katika mtandao wake.


Akaunti ya Dahir katika mtandao wa kijamii wa LinkedIn inasema alikuwa anapenda sana kupiga picha na "kuangazia kuhusu watu walio katika hatari hususan waathiriwa wa vita wasiokuwa na sauti, katika kuuelimisha ulimwengu kuhusu athari kubwa za vita".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad