Ili timu ya taifa iwe bora, tunahitaji kuwa na vilabu bora, Lengo letu Simba sio kushindana na timu za nyumbani pekee” – Mo Dewij

Ili timu ya taifa iwe bora, tunahitaji kuwa na vilabu bora, Lengo letu Simba sio kushindana na timu za nyumbani pekee” – Mo Dewij
Mmoja ya wamiliki wa simba na C.E.O wa kampuni ya METL Mohamed Dewij amefunguka na kuonyesha nia yake na ya klabu ya Simba kwa ujumla.


Baada ya timu hiyo kupata matokea nyumbani katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya timu kutoka nchini Algeria ya JS Saoura, tayari ameweka wazi mipango yao hasa kuelekea katika mchezo wa leo jioni dhidi ya timu kutoka nchini DR Congo ya AS Vita club.


Kwenye ukurasa wake wa Instagram Mo ameandika:- ” Ili tuwe na timu ya taifa bora, tunahitaji kuwa na vilabu bora. Na sisi shabaha yetu kwa SIMBA sio kushindana tena na timu za nyumbani pekee, lazima sasa tukashindane na vilabu vingine vikubwa vya Afrika. Ukubwa wetu usiishie kugombea ubingwa wa Tanzania tu.”


Ikumbukwe kwamba katika kundi hilola michuano ya klabu bingwa barani Afrika Simba wako kundi D na timu nyingine kama Al ahly, JS Saoura, AS Vita club na Simba yenyewe.


Katika kundi hilo tayari anaongoza Al ahly akiwa na alama 4 na michezo miwili baada ya mchezo wao wa jana usiku kupata sare ya goli 1-1 dhidi ya JS Saoura.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad