Rais mstaafu wa Afrika Kusini Jacob Zuma, anakusudia kuingia studio hivi karibuni, kurekodi albam ambayo itakuwa na nyimbo za mapambano.
Taarifa hiyo imetolewa na Thembinkosi Ngcobo ambaye ni Mkuu wa Hifadhi ya Utamaduni na Burudani, na kusema kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya kuona hakuna msanii wa sasa anayeimba nyimbo za mapambano, kama zamani.
“Tulikuwa tunatafuta wasanii wa nyimbo za aiana hii, ilikuwa ngumu , tulijaribu kutafuta hata video fupi fupi, lakini hatukupata kitu katika jumba la makumbusho, hapo ndipo kama Idara tukamkumbuka Zuma kwenye sula la kuimba”, ameeleza Ngcobo.
Akiendelea kuelezea hilo Ngcobo alisema kwamba, ”Hivi karibuni tulikuwa na Mazungumzo na Zuma, tulienda nyumbani kwake, tukajadili, alianza kuongelea mengine lakini kabla hatujaondoka, alisema amefurahi kuwa sehemu ya 'ptoject' hiyo, hivyo tutaangalia namna ya yeye kufanya mazoezi na kwaya hivi karibuni".
Iwapo Rais Jacob Zuma ataingia studio na kurekodi album hiyo, atakuwa Rais wa Pili afrika kuweka wazi uwezo wake wa kufanya muziki, baada ya Rais Yoweri Musevi wa Uganda, ambaye ameshawahi kusikika akirap.