Mahakama hiyo ilimwachia huru Mhando na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye alisema sababu za kumwachia huru kuwa ni mikataba minne aliyoingia haikuwa na nguvu ya kisheria kwani haikusainiwa na wahusika akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Hata hivyo, Wakili wa Serikali Leonard Swai alidai kuwa Jamhuri haujaridhika na hukumu hiyo kwamba pamoja na kwamba mikataba inadaiwa kuwa haikufuata sheria lakini mawakili walilipwa fedha,hasara ambayo imesababishwa na na mshtakiwa.
Rufaa hiyo inasubiri kupangiwa jaji na tarehe ya kusikilizwa.
Katika kesi hiyo Tido alikuwa anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 887.1.