Jeshi la Polisi Dar latuhumiwa


Katibu wa Baraza la Vijana la CHADEMA Mkoa wa Kichama Temeke, Hilda Newton amelalamikia kitendo cha jeshi la polisi kumnyemelea, kukamata na kuwaweka kizuizini ndugu zake mpaka pale watakapomkamata.


Katika madai yake, Hilda amesema kwamba Januari 18, 2019 alipewa taarifa ya kuaminika kuwa kuna askari walisafiri kutoka Dar kwenda Iringa kwa lengo la kumtafuta, huku wakiwaweka kizuizini ndugu zake.

Ameeleza kwamba "nimeshangaa inakuaje mtu ambae ni mkazi wa Dar es salaam alafu Polisi wanatoka Dar wanaenda kunitafuta kwa kunivizia Iringa" ?

"Nakumbuka Februari 2015 wakati naratibu maandamano ya Bavicha Dar es Salaam kuhusu zoezi la BVR Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam liliniandikia barua na kunitaka nifike ofisini kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam niliitikia wito tukazungumza na Kova baadaye nikaenda nao mpaka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Lubuva tukafanya kikao mwisho wa siku tukaafiki kusitisha maandamano yetu" Amesema.

Hata hivyo kiongozi huyo wa Vijana CHADEMA amewafahamisha wazazi wake kuwa usalama wake upo chini ya jeshi la polisi kutokana na namna anavyotafutwa kwa kuviziwa.

"Napenda kuwambia wazazi wangu, Viongozi na Wanachama wa CHADEMA, ndugu jamaa na marafiki kama likinikuta jambo lolote baya iwe kupigwa, kutekwa au kupotezwa hakika Jeshi la Polisi Tanzania ndo watakao kuwa na majibu na kujua mhusika ni nani" ameeleza.

Hata hivyo hivi karibuni, Hilda alijikuta kwenye matatizo na Mkuu wa mkoa wa Iringa, Ally Hapi baada ya binti huyo kuchapisha tuhuma mtandaoni juu ya kulazwa makaburini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad