Jinsi Joseph Kabila Alivyopiga Chenga ya Mwili, Akili za Wapinzani na Mataifa ya Nje


Jana tume ya uchaguzi Nchini nKongo (CENI) ilimtangaza FELIX TSHISEKEDI kutoka chama cha Upinzani cha UDSP kuwa mshindi wa kiti cha Urais baada ya kupata kura milioni 7, akifuatiwa na MARTIN FAYULU kura milioni 6.4 aliyekuwa akiwakilisha Muungano wa vyama vya Upinzani huku mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na Rais anayemaliza muda wake EMMANUEL SHANDRY akiambulia milioni 4.4.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, wafuasi wengi wa vyama vya Upinzani Nchini Kama ambavyo ilitarajiwa hawakusita kuonesha furaha zao kupitia mitandao mbalimbali kwa hoja kubwa kwamba chama tawala kimeondoka madarakani na wengine kwenda mbali zaidi na kusema 'Kabila habari yake imekwisha'

Kwa wafuatiliaji na wachambuzi waandamizi wa masuala ya kisiasa hasa za Kiafrika watakubaliana nami kwamba kilichofanyika ni Rais aliyeondoka madarakani KABILA kupiga chenga ya mwili akili za Wapinzani nchini Kongo na Afrika kwa ujumla sambamba na Mataifa ya nje ambayo kila kunapokucha hayapendi kuona taifa hilo likiwa katika hali ya amani na utulivu kwani kunaweza kuwa kikwazo kikubwa katika wizi wa madini yaliyojaa tele katika taifa hilo la Afrika ya kati.

kabila alipigaje hiyo chenga ya mwili?

Kutafuta mshindi ambaye atalinda maslahi yake binafsi na watu wa Kongo, ikumbukwe kanisa katoliki nchini Kongo na Ufaransa kwa nyakati tofauti yameeleza Mgombea aliyekuwa anawakilisha umoja wa Upinzani FAYULU ndiye aliyeshinda uchaguzi huo, Kama huo ndio ukweli ni wazi baada ya Kabila kubaini mgombea wake(SHANDRY) ameshindwa huku FAYULU akiwa na kura nyingi, akifuatiwa na TSHESEKEDI alichokifanya ni kuchagua shetani moja kati ya wawili( rejea theory of the lesser evil) na kwa mazingira yalivyokuwa akaamua kumtangaza TSHESEKEDI kuwa mshindi akiamini msimamo wake dhidi yake(kabila) ni AHUENI ikilinganishwa na FAYULU ikumbukwe kuwa TSHISEKEDI alikuwa tayri na uhasama na umoja wa vyama vya Upinzani ukiongozwa na FAYULU baada ya kumzuia kupeperusha bendera ya umoja huo licha ya kuwa maarufu na wafuasi wengi.

Ni nini kimetokea na kitatokea baada ya chenga hiyo ya mwili?

i) wananchi, vyama vya Upinzani na wakosoaji wakubwa wa kabila sambamba na mataifa ya nje yaliyokuwa yanampiga hayaongei lugha moja yanapingana yenyewe badala ya Kabila!!!!!!!

ii)Ni vigumu sasa kwa mataifa ya nje kutoa mashinikizo kwa tume ya uchaguzi kurudia uchaguzi zaidi ya kukosoa mwenendo wa uchaguzi haukuwa wa haki n.k kwanii bado aliyeshinda ni kutoka Upinzani Kama mataka ya awali ya Nchi hizo.

iii)TSHESEKEDI ataapishwa na kulinda maslahi mapana ya wakongomani pamoja na yale ya Kabila.

Kabila katoa funzo kubwa kwa Afrika kwamba tunaweza kulinda maslahi yetu mapana ya wananchi wetu pasipo kuleta kusababisha umwagaji damu, vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo hutoa fursa kwa mataifa ya nje kuvuruga amani na utulivu wa nchi zetu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad