Jinsi shambulizi la Kenya lilivyoigusa Tanzania

Jinsi shambulizi la Kenya lilivyoigusa Tanzania
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wameoneshwa kuguswa na tukio la shambulizi eneo la ofisi la 14 Riveside Jijini Nairobi Kenya ambalo lilipelekea watu 14 kufariki duniani kwenye tukio hilo.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliandika kuwa amefanya mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata na kumpatia salamu za pole juu ya tukio hilo la kusikitisha.

"Nimezungumza na Kenyatta kuhusu shambulizi la Jijini Nairobi, Pole sana Rais na pole sana wananchi wa Kenya. Tupo nanyi katika kipindi hiki cha majonzi. Nawaombea marehemu wote walale mahali pema peponi, Amina. Tuko imara".ameandika Rais Magufuli

Pia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia Afisa Habari wake wametoa taarifa ya kusikitishwa na tukio hilo pamoja na kumpa salamu za pole Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata na kuviomba vyombo vya usalama nchini humo kuhakikisha majeruhi wa wanapona kwa haraka.

"Kipekee CHADEMA inatuma salaam za pole kwa watu wote walioathiriwa na tukio hilo, kwa kupoteza maisha ya wapendwa wao na wengine waliojeruhiwa, tunawatakia majeruhi wote uponaji wa haraka,Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano", ilisema taarifa hiyo ya CHADEMA.

Juzi wakati tukio hilo linatokea, wasanii na watu mbalimbali maarufu nchini, kupitia mitandao ya kijamii, walionesha kuguswa na tukio hilo, hususani wasanii wa muziki ambao mara kwa mara wamekuwa wakielekea nchini humo kwa ajili ya kufanya matamasha mbalimbali.

Miongoni mwa wasanii hao Joh Makini, Baraka De Prince, Alikiba, Ay. Jux, Maua Sama

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad