Mkali wa Bongo Flava, African Boy “Juma Jux” amedondoka Coke Studio Africa kwa mara ya kwanza akiwa anatamba na mikwaju kadhaa Afrika ya Mashariki kama vile.
“Zaidii” na “Tell Me”. Ukiachana na mziki, Jux pia ni mfanyabiashara akiwa ni mmiliki wa chapa ya T-shirts “AFRICAN BOY”, ni bidhaa za nguo zinazopatikana Afrika Mashariki zikimilikiwa na mwimbaji pamoja na mtunzi Juma Jux.
Ameeleza kuwa moja ya mipango yake kwa mwaka 2019 ni kufanya nyimbo nyingi za kushirikiana na wasanii kutoka nje ya Tanzania. Katika Coke Studio Jux anashirikiana na mwana dada Shellsy Baronet kutoka Mozambique.
Juma Jux anaelezea mengi kuhusu mara ya kwanza kwake Coke Studio Africa, “Coke Studio ni jukwaa zuri kwa wasanii kwani inapelekea kubadilishana tamaduni na nchi zingine; ni kitu kizuri ambacho nafurahi kuwa sehemu ya Coke Studio.” Juma Jux
Wawili hao wametengeneza bonge la collabo katika lugha ya Swahili, Portuguese na Kiingereza itakayoongelea mapenzi
Jux amekuwa ni moja ya wasanii waliofanya vizuri sana mwaka 2018 kwa kuachia nyimbo nyingi zilizofanya vizuri, pia pamoja na Vanessa Mdee waliweza fanya tour kubwa “In Love & Money” katika mikoa ya Tanzania. Jux pia amefanikiwa kuwa moja ya wasanii wenye bidhaa zilizofanya vizuri kwa mwaka 2018 “AFRICAN BOY”. Atafanya vizuri zaidi akiendelea na utaratibu huu wa kuachia nyimbo nzuri kwa mwaka 2019.
JUMA JUX ataiwakilisha vyema chapa ya “AFRICAN BOY” katika jumba la Coke Studio kwa mwaka 2019, kuanzia Februari.