Muimbaji Gigy Money amesema mapenzi ya kweli ni wawili kuvumiliana ndio sababu hadi leo yupo na mpenzi wake Mo J licha ya kutofautia mara kwa mara.Gigy Money ameeleza hayo wakati akipiga stori na kipindi cha social buzz cha Clouds TV.
"Mliyoko kwenye mapenzi leo kama mwanaume hana hela, kakulaza njaa, hayo ndio mapenzi, hiyo ndio kupanda na kushuka na wasichana si ndio tunajifanya tunapenda mapenzi, kwa hiyo kama unapenda mtu muonyeshe shida zako na raha zako," amesema Gigy Money.
Licha ya kufanya muziki na video vixen, Gigy Money kwa sasa ni mama wa familia.