Alinusurika Shambulio la Osama Marekani, Ameuawa na Al Shabaab Kenya


ALIYENUSURIKA katika shambulizi la kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani, ni miongoni mwa watu zaidi ya 20 waliouawa na magaidi kwenye jengo lenye hoteli ya Dusit 2, Riverside jijini Nairobi nchini Kenya.

Kijana huyo mfanyabiashara raia wa Marekani, anajulikana kwa jina la Jason Spindler na ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya I-Dev International.  Mtu huyo alinusurika katika shambulizi lililofanywa na kundi la kigaidi la Al-Qaeda likiongozwa na Osama Bin Laden, baada ya ndege zilizotekwa kubamizwa kwa makusudi kwenye majengo mawili jijini Washington DC na New York ambapo watu 3,000 walipoteza maisha.

Mama yake Spindler ameliambia Shirika la Habari la NBC kuwa wamesikitika kumpoteza kijana wao ambaye alikuwa na umri mdogo. Taarifa ya kitengo cha Ubalozi wa Marekani nchini Kenya imethibitisha kuwa raia wa Marekani ni mmoja kati ya watu waliouawa kwenye shambulizi hilo la Nairobi lakini haikutoa taarifa zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad