Kesi Ya Zitto Kabwe Yapigwa Kalenda Hadi January 29

Kesi Ya Zitto Kabwe Yapigwa Kalenda Hadi January 29
Kesi ya 'uchochezi' inayomkabiili Mbunge wa Kigoma Mjini, Zito Zuberi Kabwe imeahirishwa mpaka Januari 29, itakapoitwa kwa ajili ya kwenda kusikilizwa

Kesi hiyo  ya Jinai namba 327 ya Mwaka 2018 inayomkabili Kiongozi huyo leo tarehe 14 Januari 2019 katika Mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es salaam ilifika kwa ajili ya kutajwa na kutolewa maamuzi ambayo yalitolewa na Hakimu Mkazi, Janeth Mtega baaada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili (Mashtaka na utetezi).

Upande wa Mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Adolf Kissima  ulidai kwamba kesi hiyo leo ilikwenda kwa ajili ya kutajwa lakini upande wa mashtaka hawakuwa na jalada halisi la kesi hiyo.

Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili wa Zitto, Steven Mwakibolwa uliikumbusha mahakama kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na mahakama hiyo kupitia Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama, Huruma Shaidi na ilishapanga tarehe ya kuanza kusikilizwa, ambayo ni Januari 29, 2019.

Inadaiwa kuwa Oktoba 28,2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo, kiongozi huyo alitumia maneno yenye kuleta kuleta chuki miongoni mwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la Polisi.

Mbunge huyo alifikishwa Mahakama ya Kisutu kwa mara ya  kwanza, Novemba 2, 2018, bado anaendelea na dhamana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad