Kesi za uchaguzi Yanga kufutwa, mchakato kuendelea

Kesi za uchaguzi Yanga kufutwa, mchakato kuendelea
Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kupitia kwa Mwenyekiti wake Malangwe Ally Mchungahela, imeeleza kuwa wanachama waliokuwa wamefungua kesi mahakamani wamekubali kuondoa kesi hizo.
Akiongea leo jijini Dar es salaam, Mchungahela amesema walibaini kuwa baadhi ya wanachama waliopeleka mahakamini kesi ya kupinga uchaguzi, wengi wao uanachama wao una dosari isipokuwa mmoja tu.

''Kamati ilipitia malalamiko yote hayo kwa kina na kuwapelekea ujumbe walalamikaji wote kwamba uanachama wao Yanga una hitilafu ki-Katiba, hivyo hawakuwa na sifa ya kupeleka malamamiko yao popote pale kwa kivuli cha uanachama wa klabu'', ameeleza Mchungahela.

Aidha amefafanua kuwa walalamikaji wote wameelewa na wamekubali kuondoa kesi zao zote mahakamami ili kutoa mwanya kwa uchaguzi kuendelea.

Mchungahela amesema Kamati itawasilisha TFF malalamiko yote ya wanachama hao ili yafanyiwe kazi ndani ya siku 7 kuanzia Januari 14, 2019 na baada ya hapo Kamati itatangaza ratiba ya kukamilisha uchaguzi mdogo wa Yanga.

Uchaguzi huo ni mdogo kwaajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na viongozi waliojiuzulu. Viongozi watakaochaguliwa watakaa madarakani kwa takribani mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad