Kiatu cha Kigwangalla Alichovaa Ikulu Chawa Gumzo

Kiatu cha Kigwangalla Alichovaa Ikulu Chawa Gumzo
Kwa siku ya pili mfululizo tangu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla alivyofanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu, kumekuwa na gumzo juu ya kiatu alichovaa katika mazungumzo hayo.


Rais Magufuli akitoka Ikulu pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega

Januari 15, Waziri Kigwangalla alialikwa na Rais Magufuli kufanya mazungumzo Ikulu Jijini Dar es salaam, lakini mshangao wa wengi ni katika picha alipokuwa akitoka nje na Rais Magufuli, iliyoonesha kiatu chake kikiwa na vumbi kali lililoziba rangi ya kiatu hicho.

Mwenyewe amesimulia namna mazingira yalivyokuwa hadi kupelekea kiatu chake kufunikwa na vumbi ilhali alikuwa ameitwa na Rais Ikulu.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kigwangalla ameandika kuwa.


@HKigwangalla
 Nimevaa zangu jeans na shati nasafiri kwenda field Mikumi National Park; ghafla wito wa Ikulu, natupia kaunda suti ya dharura, kucheki sina moka, kuna mabuti/sneakers na siwezi kuhangaika kununua mpya, nkapiga buti nikaitika wito ndani ya muda! #RealMenWearBoots 😀#MzeeWaField

azungumzo na Rais Magufuli Ikulu, sambamba na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamuhanga, aliandika.

@HKigwangalla
 IKULU, Mapema leo: Mhe. RAIS: Hongera, naona unataka kwenda Zanzibar...umepata? KIGWANGALLA (akicheka): Ahsante Mhe., si unaona ni ‘keupe’? Mhe RAIS (akicheka): Tena wewe si unaruhusiwa wanne? KIGWANGALLA: Kabisa Mhe., bado nina nafasi tatu! 😀


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad