Kibadeni Awaombea Ajira Wakongwe wa Simba

Kibadeni awaombea ajira wakongwe wa Simba
Ikiwa tayari tumeshauanza mwaka 2019, leo Jumanne, mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba, Abdallah Kibadeni amesema ana imani ya timu yake kuongoza ligi endapo itashinda michezo yake yote ya viporo pamoja na mechi dhidi ya Yanga.

Kibadeni ameyasema hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv juu ya kiwango cha Simba katika mashindano mbalimbali mwaka 2018 ambapo amesema kuwa suala la kumfunga Yanga liko pale pale na ni lazima Simba irejee kuongoza ligi.

Pia mkongwe huyo ambaye aliwahi kufundisha klabu ya Simba, ameuomba uongozi wa klabu hiyo kuwakumbuka wakongwe ambao wameipigania klabu mpaka hapa ilipofikia kuwapa nafasi zozote zitakazowalea.

"Ninachotaka kusema kwa wanasimba na uongozi kwa ujumla, wasiwatupe watu ambao wameifikisha klabu pale ilipo kwasababu hivi sasa wanatupwa na wanasahaulika," amesema Kibadeni.

"Watu wenyewe nikianza na mimi mwenyewe, Hamis Kilomoni, Khalid Abeid, Mike Baraza na wengineo wengi ambao wakati wakicheza walitoa jasho bila kulipwa mishahara. Kama kuna ajira ndogo ndogo wapewe hata kazi yoyote pale ofisini wakae, itasaidia kuleta baraka ndani ya klabu," ameongeza.

Aidha, Kibadeni amesema kuwa ana dawa ya kuwamaliza Waarabu (Al Ahhy) ambao wamepangwa na Simba katika kundi moja michuano ya Klabu Bingwa Afrika na kuitaka Simba iwaone wakongwe kama yeye kwakuwa wana siri nyingi za timu kutoka Afrika ya Kaskazini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad