BAADA ya swali la wapi anapotoa jeuri ya fedha muigizaji Irene Uwoya kugonga vichwa vya watu wengi kwa muda mrefu, hatimaye siri imefichuka baada ya Ijumaa Wikienda kuelezwa mhusika!
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kipo karibu na msanii huyo, jeuri hiyo anaipata kutoka kwa kigogo mzito aliyepo kwenye Serikali ya Kenya.
“Ni kigogo (anamtaja jina, tunalihifadhi sababu hatujampata kuthibitisha) katika Serikali ya Kenya, ndiye ambaye anamuwezesha kwa kila kitu. Hizi sijui kufuru za bethidei yake, sijui kujiachia kwenye boti hadi Zanzibar kigogo huyo ndiye anayemuwezesha,” kilidai chanzo hicho.Chanzo hicho makini kilizidi kwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa, kutokana na uzito wa kigogo huyo, imekuwa ngumu kujulikana na hata anayejua pia huhofia kusema.
“Ni kutokana tu na uzito wa kigogo huyo na bahati mbaya sana ni kwa sababu yupo Kenya, ingekuwa yupo Bongo ingekuwa ni rahisi sana watu kumjua,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Kigogo huyo ndiye anayedhamini pia zile safari za mara kwa mara za Uwoya nchini Dubai, nafikiri huwa wanakutania huko na huyo kigogo kula zao raha.”
Baada ya gazeti hili kupata habari hiyo lilimtafuta Uwoya na kumuuliza kuhusiana na madai hayo ambapo alifunguka kama ifuatavyo:
Ijumaa Wikienda: Hebu tuweke wazi, tumeelezwa kuwa jeuri uliyonayo ya fedha kwa sasa hivi unapewa na kigogo wa serikalini nchini Kenya (anatajiwa jina la kigogo) je ni kweli?
Uwoya: (Kicheko) Hivi kwa nini kila mtu anapenda kumjua mtu wangu maana marafiki wanapenda kumjua, wasanii wenzangu, mpaka ndugu zangu yaani watu wanahangaika kweli jamani.
Ijumaa Wikienda: Sawa ila tunataka kufahamu ukweli ni upi?
Uwoya: Huyo (anamtaja jina) nampenda sana labda niseme hivyo, siku akija Bongo watu watafunga midomo yao.
Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo unatuthibitishia kuwa ni mpenzi wako au vipi?
Uwoya: Mtajua muda muafaka ukifika na hata akiwa sio pia mtajua baadaye.
Siku za hivi karibuni, Uwoya amekuwa akiponda raha na kundi la mastaa wenzake katika viunga mbalimbali vya starehe huku ikielezwa yeye ndiye anayesimamia mpango mzima wa starehe, hivyo watu wengi kuhoji aliyeko nyuma yake.
Stori: Imelda Mtema,Dar