mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi walioandamana katika baadhi ya mitaa wakiwa na madai ya kutaka ‘wamshughulikie’ mtu alinayedaiwa kuwa ni mtekaji na muuaji wa watoto mkoani humo.
Tukio hilo limetokea leo Jumanne, Januari 29, 2019, ikiwa ni siku moja baada ya mazishi ya watoto watatu wa familia moja ambao walikutwa wameuawa baada ya kudaiwa kutekwa na watu wasiojulikana mkoani humo kisha watano kupatikana ambapo watatu walikuwa wa familia moja ambao walitambuliwa na ndugu zao huku wawili wakishindwa kutambulika na kuzikwa na Manispaa.
Wananchi hao wamedai kuchoshwa na matukio hayo ya utekaji ambapo inaelezwa kwa kipindi cha mwezi mmoja, watoto 10 wametekwa huku wengine wakiuawa na wengine hawajuliakni walipo mpaka sasa lakini chanzo cha utekaji kikiwa hakijulikani wala mtekaji akiwa hajakamatwa.
Aidha, wakati wa mazishi ya watoto hao jana, msoma risala alidai watoto hao walichukuliwa na mtu nyumbani kwao, wakati wakichukuliwa walikuwa watano; “Watoto waliobaki walipoulizwa wenzao wako wapi walisema wamechukuliwa na Joely Nziku,” alisema msoma risala huyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni alisema serikali itachukua hatua kali kwa watakaobainika ili iwe fundisho kwa wengine. Lakini pia leo Masauni amekutana na wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe katika viwanja vya Turbo na kuahidi kupambana kikamilifu juu ya mauaji ya watoto yanayoendelea mkoani humo.
Masauni amethibitisha kukamatwa kwa baadhi ya wahusika wa mauaji ya watoto mkoani Njombe na msako zaidi unaendelea ili wote waliohusika waweze kuwabaini na kutokomeza kabisa mauaji hayo huku akiwataka wananchi kuwa watulivu na kutojichukulia sheria mkononi.
“Niwahakikishie vyombo vyenu vya usalama viko imara na nimewaagiza wahakikishe matendo haya ya kinyama yanaisha haraka sana. Tumeendelea kuimarisha usalama wa mataifa mengine hii ni kwa sababu nchi yetu ina amani, tumezima majaribio ya uvunjifu wa amani, sasa natoa salaam waovu hawa wanaofanya vitendo hivi katika maeneo haya ya Njombe hawatabaki salama,” amesema Masauni.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka, ameagiza msako wa waganga wa kienyeji na kuwakamata baadhi yao ikiwa ni hatua ya kutafuta watuhumiwa wa makosa ya kutekwa na kuaawa watoto mkoani humo ambapo hivi karibuni iliripotiwa watoto tisa walitekwa na kuawa.
Kimenuka Njombe Mabomu Yarindima Kutawanya Wananchi
0
January 29, 2019
Tags