Mbunge wa Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete amesema bado Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala hajafanya kazi yake vilivyo katika kutangaza vivutio vya utalii nchini.
Ridhiwani ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 3, 2019 katika uzinduzi wa redio ya kutangaza utalii ya 'Hakuna Matata'.
Amesema hivi karibuni alimuona Dk Kigwangalla akipiga picha katika moja ya mbuga za wanyama kama moja ya njia ya kuhamasisha kutembelea vivutio vya utalii.
"Nilipoiona picha ile, nilimkosoa kwa kweli na kumwambia bado hajaweka nguvu kubwa kwenye ushawishi, ingekuwa vizuri kama angetumia wasanii ambao wana watu wengi wanaowafuatilia kwenye mitandao ya kijamii," amesema Mbunge huyo
Kuhusu ujio wa redio hiyo, Ridhiwani amesema ni jambo zuri ukizingatia kuwa ni ya mtandaoni ambako dunia imehamia huko.
Awali akieleza lengo la kufungua , Mkurugenzi wa redio hiyo, Beatrice Ndungu, amesema moja ya sababu ni kutangaza utalii na pia kuzalisha ajira kwa vijana.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wasanii mbalimbali akiwemo Miss Tanzania, Elizabeth Makune, Mzee Chilo na Monalisa,.
Hajamvaa bali ametoa mchango wake kimawazo ili kuboresha utalii nchini. Ni kweli pesa nyingi zielekezwe kwenye utangazaji, utumiaji wa watu maarufu duniani katika kuutangaza utalii wa Tanzania utaweza kuvuta wageni wengi zaidi. Pia uanzishaji wa mfumo wa kutoa commission kwa kila atakaye leta idadi fulani ya watalii nchini, inaweza kuchangia ongezeko la watalii na pia ajira kwa watanzania hao waletao watalii, hii itawahusu hata wale watanzania waishio nje ya nchi
ReplyDelete