Kiongozi Yanga atoa pongezi kwa Simba


Aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa Yanga na hivi sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro, amewapa pongezi Simba baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Muro ameandika hayo katika ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa hatua waliyofikia Simba imewatoa kimasomaso watanzania wote baada ya ushindi huo. 

"Tuna kila sababu ya kusimama pamoja kama taifa na kuipongeza sana Simba, hakika mmetutoa kimasasomaso watanzania, ndugu yangu Haji Manara hongera, hamasa yako imekuwa chachu ya matokeo mazuri uwanjani. This Is Amazing And Fantastic" - alisema Muro 

Aidha, Muro amempongeza Msemaji wa Simba, Haji Manara kwa namna anavyojitoa kutia hamasa na morali kwa mashabiki wa Simba na kuwa sababu au chachu ya matokeo mazuri. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad