Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Sasha alisema kuwa anamshukuru Mungu mwaka ameuanza vizuri kwani amepewa gari aina ya Toyota Harrier (New Model) na mwanaume huyo ambaye pia amemuahidi kumuoa.
Sasha alipotakiwa kumuonesha mwanaume huyo kwa picha aliingia mitini na kudai kuwa kwa sababu ni waziri hawezi kumuanika kwa sasa.
“Unajua huyu ni waziri mimi naona sio vema kumuanika kwa jina ila kwa sababu ana nia ya kunioa, mtamuona hivi karibuni kwani mambo ya kuficha ficha hayatahitajika tena,” alisema Sasha.
Sasha ndani ya miaka miwili ameshahaidiwa kuolewa na wanaume watatu tofauti wakiwemo wanaume wa nje ya nchi lakini mpaka tunavyoandika habari hii, hakuna hata aliyemvisha pete ya uchumba zaidi ya kumdanganya na kuingia mitini.
NENO LA MHARIRI
Sasha ni msichana mrembo ambaye akitulia na kuwa na uhusiano wa kueleweka anaweza kuolewa na kuwa mama bora hivyo Ijumaa Wikienda linamsihi kuwa na uhusiano sahihi wenye msimamo thabiti.
STORI: Hamida Hassan, Ijumaa Wikienda