Kocha wa Simba atoa tamko Baada ya Kutolewa SportPesa

Kocha wa Simba atoa tamko Baada ya Kutolewa SportPesa
Kocha mkuu wa klabu ya Simba Patrick Aussems amesema hawana budi kukubali kuwa wametolewa kwenye michuano ya SportPesa Cup 2019.

Aussems ameweka wazi kuwa kinachotakiwa sasa ni kuangalia mbele katika mechi zijazo za michuano mbalimbali wanayoshiriki.

''Tumetolewa licha ya kucheza vizuri na kutengeneza nafasi, tunatakiwa kutazama mechi zijazo za ligi kuu na Ligi ya mabingwa Afrika'', alisema Aussems kupitia taarifa iliyotolewa na klabu hiyo.

Simba jana Januari 25, ilitupwa nje ya michuano ya SportPesa kwa kufungwa mabao 2-1 na Bandari FC ya Kenya katika hatua ya nusu fainali.

Simba sasa inajiandaa na mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi D dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaopigwa Februari 2 huko Misri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad