Kundi la Al-Shabaab Lakiri Kutekeleza Shambulizi la Kigaidi la Westlands, Kenya

Kundi la kigaidi la Al-Shabaab Lakiri Kutekeleza Shambulizi la Kigaidi la Westlands, Kenya
Msemaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabab amekiri wazi kuwa, milipuko na milio ya risasi iliyotokea katika Hoteli ya Dusit mapema mchana wa leo huko Westlands jijini Nairobi nchini Kenya, limetekelezwa na kundi hilo.


Msemaji huyo ameliambia Shirika la Habari la BBC kwa njia ya simu, kuwa kundi hilo ndio lililotekeleza shambulizi hilo.

Hata hivyo, Msemaji huyo hajatoa maelezo zaidi, lakini amesema kundi hilo litatoa maelezo zaidi punde operesheni yao ikikamilika.

Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote rasmi ya vifo kwenye shambulizi hilo la kigaidi .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad