WAMILIKI wa simu zinazotumia programu endeshi ya simu aina ya Series 40 wamekuwa hawawezi tena kutumia mtandao wa WhatsApp kwenye simu zao.
Hiyo imetokana na uamuzi wa kampuni ya Facebook inayomiliki mtandao wa kijamii wa WhatsApp wa kuacha kutengeneza app yake kwa njia ambayo inaweza kutumiwa katika simu hizo.
Wengi zaidi wataathirika katika kipindi cha mwaka ujao, 1 Februari, 2020 ambapo simu nyingi zikiwemo baadhi ya iPhone zitapoteza uwezo wa kutumia WhatsApp.
Hata kabla ya wakati huo kufika, Facebook wameonya kwamba “kwa sababu hatutakuwa tukitengeneza na kuboresha app yetu tukizizingatia, huenda baadhi ya uwezo wake ukaathirika wakati wowote.”
Zitakazoathirika mwaka ujao ni za Android zinazotumia Android 2.3.7 na miundo ya awali, pamoja na iPhone zinazotumia iPhone iOS 7 kwenda nyuma. Kwa sasa, mfumo wa Android umefikia 9.0. [Unaweza kuangalia mfumo unaotumiwa na simu yako kwenye ‘Settings’, kisha sehemu ya ‘Software/Software Info]
Wanaotumia Android 2.3.7 kwenda nyuma hawawezi kufungua akaunti mpya za WhatsApp.
Ili uweze kutumia mtandao huo kwa sasa unahitajika kuwa unatumia Android 2.3.3 kwenda juu na Windows Phone 8.1 kwenda juu.
Kwa sasa, walioathirika zaidi ni wanaotumia baadhi ya simu za Nokia zinazotumia mfumo endeshi wa Series 40 ambao wakati mwingine huitwa S40 OS. Miongoni mwa simu maarufu zilizoathirika ni Nokia 6300.
Simu ya mwisho kutegenezwa ambayo ilikuwa inatumia S40 ilikuwa Nokia 515 ambayo ilizinduliwa mwaka 2013.
Ingawa baadhi ya simu hizi ni za bei nafuu na hutumiwa na watu wa kipato cha wastani au cha chini, kuna wanaotumia simu aina ya pia simu za Vertu Signature S ambazo zilikuwa ghali sana na ambazo hutumia programu hiyo endeshi pia.
Wakati wa kuanza kuuzwa kwa simu hizo zilikuwa zinauzwa takriban £8000 (Tshs23m; Kshs1m), ingawa hiyo ilikuwa miaka kumi iliyopita na huenda wengi wao wamenunua simu nyingine au wana uwezo wa kununua simu nyingine kwa urahisi.
Simu Ambazo Zimefungiwa Whatsapp kuanzia Tarehe 1, 2019
Nokia 206 Single SIM na dual SIM
Nokia 208
Nokia 301 Single SIM na dual SIM Chat Edition
Nokia 515 zinazouzwa zikiwa na WhatsApp
Nokia Asha 201
Nokia Asha 205 Chat Edition
Nokia Asha 210
Nokia Asha 230 Single SIM na dual SIM
Nokia Asha 300, 302, 303, 305, 306, 308, 309, 310, 311
Nokia Asha 500, 501, 502, 503
Nokia C3-00
Nokia C3-01
Nokia X2-00
Nokia X2-01
Nokia X3-02
Nokia X3-02.5
Kufikia Juni mwaka 2017, huduma ya WhatsApp pia ilikuwa imeacha kutumika tena katika aina kadha za simu za zamani zikiwemo zile zilizotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6.
Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo ilisema wakati huo kwamba inataka kuangazia kustawisha “huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi.”
Kampuni hiyo ilikuwa imeorodhesha simu za BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60 kuwa miongoni mwa simu ambazo zingekatiwa huduma mwishoni mwa mwaka 2016 lakini ikabadilisha uamuzi wake na kuongeza muda hadi Juni 30, 2017.
Simu zilizotumia Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6 hata hivyo zilifungiwa mwishoni mwa 2016.
Hatua hiyo ilikuwa imetangazwa na Facebook mapema mwezi Februari mwaka 2016.
Kampuni hiyo ilijitetea na kusema kwamba haikusudii kuwatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
“Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo,” kampuni hiyo ilisema.
Mifumo Ya Simu Ambayo Haitoweza kutumia Whatsapp
Android 2.1 na Android 2.2
Windows Phone 7
iPhone 3GS/iOS 6
BlackBerry OS and BlackBerry 10
Nokia S40
Nokia Symbian S60
Wanaotumia simu zilizofungiwa wameshauriwa kununua simu za kisasa zaidi. Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia. Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.
List ya Aina ya Simu Zilizofungiwa Kutumia Whatsapp Mwaka 2019...Angalia yako Kama Ipo
0
January 03, 2019
Tags