Lugola Afunguka Kuhusu Polisi Aliowatumbua Kuendelea Kufanya Kazi

Lugola Afunguka Kuhusu Polisi Aliowatumbua Kuendelea Kufanya Kazi
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema alishatoa maagizo ya kuondolewa kwenye nyadhifa zao kwa makamanda wa Polisi wa Mikoa mitatu ya Kipolisi nchini ambayo ni Temeke, Ilala na Arusha, hivyo imebaki kutekelezwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro.



“Sina taarifa kuhusu agizo langu kutotekelezwa, lakini kwa vile nilimpa muda wa utekelezaji IGP, ninaamini litatekelezwa, saa nyingine watu hawajui kutengua mtu ni mamlaka na mimi ndiye nina mamlaka, utekelezaji ndiyo unaendelea sidhani kama wamekaidi au IGP amekaidi kutekeleza agizo langu,” amesema Lugola.



Jumatano, Januari 16, 2019, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Lugola alitengua uteuzi wa makamanda wa polisi wa mikoa mitatu: Salum Hamduni (Ilala), Emmanuel Lukula (Temeke) kwa kosa la kushindwa kusimamia mianya ya rushwa na utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa.

Pia alitengua uteuzi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhan Ng’anzi, kwa kumchukulia hatua askari mzalendo aliyetoa taarifa kuhusu magendo ya biashara haramu ya bangi na mirungi mkoani humo.



Kwa upande wake IGP Sirro ameshatoa ufafanuzi na kusema atafanya mabadiliko kwa mikoa hiyo hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad