Ma - DC Msicheke na Nyani Mtakuta Mahindi yote Yameondoka - RC Mwanri



Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ametoa maagizo kwa Wakuu wa Wilaya kuwasimamia watoto wa kike kwa lengo kuliokoa kundi hilo linaloathiriwa na mimba za utotoni huku akiwataka viongozi hao kutocheka na Nyani na wakicheka tu watakuta hakuna mahindi tena.

RC Mwanri ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa CHF, ambapo amewataka mabinti wanaotoka mkoani kwake watoke wakiwa na heshima, usomi na sio kuburuzwa buruzwa.

“Binti anaondoka kwa heshima sio ana buruzwa buruzwa, unakuta kabinti kadogo wameshakarukia , Wakuu wa Wilaya msicheke na nyani mtakuta mahindi yameondoka, Asharose amesomeshwa dunia yote ikaponea hapo,” RC Mwanri.

Hata hivyo, Mwanri aliwataja viongozi wakubwa ambao ni wanawake na kusoma kwao kumewafikisha walipo, akiwepo Mama Samia Suluhu, Ummy Mwalimu, Mama Samweli Sitta na wengine wengi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad