Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), imemwachia huru Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo(73), baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake
Gbagbo alifikishwa mbele ya Mahakama hiyo mwaka 2011 kutokana na vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambao ulishuhudia akishindwa mbele ya mpinzani wake, Alassane -
Gbagbo alishtakiwa kwa madai ya kuhusika na vurugu zilizosababisha mauaji ya watu 3,000 huku wengine 500,000 wakiyakimbia makazi yao
Kwa mujibu wa rekodi za ICC, Gbagbo ni kiongozi mkuu wa kwanza wa nchi kufikishwa mbele ya Mahakama hiyo.