Ameamua kukana dini yake ya Kiislamu na hajajiunga na dini nyingine yoyote. Amekimbia kuolewa. Rahaf anadai kuwa maofisa wa Saudi Arabia nchini Thailand walimpora passport yake, na wapo watu wasiojulikana ambao wanakaa nje ya mlango wa chumba cha hotel aliyomo ili asitoroke.
Anadai kuwa akirudi nchini kwake, maana wanataka kumrudisha saa chache zijazo atauawa na familia yake kwa kuwaaibisha. Wataalamu wa code of honor wataelewa maana yake na huwa wanauawa vipi kulingana na imani ya nchi aliyotoka.