Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa wanaoishi na wafanyakazi wa ndani, wanatakiwa kuona uchungu kuwatumikisha watoto wadogo wanaotakiwa kuwa shule.
Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari, ambapo amesema kuwa kukaa na mtoto mdogo na kumuagiza kazi za nyumbani ni kuitumia vibaya kodi yao kwani Rais amelipia ada watoto wote.
"Rais Magufuli amelipa ada kwa watoto wote, muwaache wasome kwani kufanya hivyo ni kuharibu kodi zenu wenyewe maana ada iliyolipwa ni kodi zenu", amesema Makonda.
Aidha katika hatua nyingine amewataka wazazi kutowapeleka watoto kujiunga na elimu ya sekondari kwa kigezo cha mahitaji, kwani walitakiwa kujiandaa mapema pindi mtoto amemaliza darasa la saba na watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua.
"Ada imelipwa na hakuna michango, lakini utakuta watu wanawaficha watoto kisa hana hela ya sare na madaftari", amesema Makonda.