Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda ameahidi kuwasweka ndani viongozi wa kisiasa ambao wamekuwa na kauli za kejeli na matusi kwa viongozi wa dini kupitia kwenye mitandao ya kijamii.
Amesema mara baada ya mkutano wa viongozi wa dini na Rais Dkt John Magufuli hivi karibuni kuliibuka mijadala kupitia mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya wanasiasa walitoa lugha za matusi na kejeli dhidi ya viongozi hao wa dini.
Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa amesema anatafuta barabara tano katika mkoa wa huo ambazo zinajengwa kwa kiwango cha lami mojawapo itapewa jina la Mwadhama Kadinali Polycap Pengo ikiwa ni njia mojawapo ya kutambua mchango wake mkubwa anaoutoa kwa nchi hii.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo wakati wa uzinduzi wa majengo ya shule ya sekondari ya mtakatifu Joseph iliyopo Goba Makonda amesema ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo barabara hiyo itakuwa imekamilika na kupewa jina la Kadinali Pengo.
Katika hatua nyingine Makonda amemwagiza afisa elimu wa mkoa kuhakikisha somo la dini zote linafundishwa katika shule zote za msingi na sekondari.