Mama Mobetto Amkingia kifua Mwanaye “Muacheni Hamisa Aishi Vile Atakavyo”

Mama Mobetto Amkingia kifua Mwanaye “Muacheni Hamisa Aishi Vile Atakavyo”
Mama mzazi wa Msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto, Shufaa Lutiginga maarufu kama Mama mobetto ameibuka na kumkingia kifua binti yake kutokana na skendo zinazomuandama.

Siku za Hivi karibuni Hamisa amekumbwa tena na skendo Mpya ya kumchukulia bwana msichana mmoj anayeitwa Tahiya.


Tahiya amemtuhumu Mobetto kwa kumchukulia Mpenzi Wake aliyetambulika kwa jina la Alex ambapo alifikia hatua ya kwenda Mpaka Zanzibar kwa ajili ya kwenda kumfumania.

Baadae Mobetto alianika picha akiwa na mwanaume huyo na kuonyesha kuwa hajamuiba bali alikuwa naye na kuwa yupo naye kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Baada ya sakata hilo Gazeti la Ijumaa lilimsaka Mama Mobetto ili kupata maoni yake juu ya skendo hizo ambako zimemuandama Mtoto Wake ambaye mara moja alimwaga Povu zito na kusema mwanaye aachwe aishi anavyopenda mwenyewe.

Jamani nilishawaambia muacheni Hamisa aishi vile ambavyo yeye anapenda, msimfuatilie siku akihitaji kuongea na nyie atawatafuta yeye mwenyewe lakini siyo kila kukicha kumfuatilia”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad