Man City Yaweka Ubingwa Rehani Baada ya Kufungwa na Newcasle, United waponea chupuchupu

Man City yaweka ubingwa rehani baada ya kufungwa na Newcasle, United waponea chupuchupu
Matumaini ya Manchester City kutetea taji lao la ubingwa wa Ligi ya Premia (EPL) kwa msimu huu yamekumbana na gharika baada ya kukubali kichapo mbele ya Newcastle Jumanne usiku.

City walisafiri hadi ugenini katika uga wa St James' Park, na waliuanza mchezo kwa kasi na kupata goli la utangulizi katika sekunde ya 24 ya mchezo kupitia mshambuliaji raia wa Argentina Sergio Aguero.

Hata hivyo ulegevu katika safu ya ulinzi ya City ulimpa mwanya Salomon Rondon katika dakika ya 66 kufunga goli maridhawa akiunganisha pasi ya kichwa kutoka kwa Isaac Hayden.

Mchezo huo ulibadili muelekeo katika dakia ya 78 baada ya Newcastle ama maarufu kwa jina la Magpies walipata penati baada ya kiungo wa City Fernandinho - kumfanyia madhambi Sean Longstaff kwenye eneo la hatari.

Matt Ritchie alisubiri kwa takriban dakika mbili kabla ya kupiga mkwaju wa penati wakati kipa wa City Ederson akipokea matibabu.

Kocha wa City Pep Guardiola na kikosi chake kina mlima mrefu wa kupanda kushusha Liverpool kileleni
Mkwaju huo ulipigwa katika dakika ya 80 na ulipeleka kilio kwa mashabiki wa City.

Hii ni mara ya kwanza kwa Megpies kuwafunga City katika Ligi ya Premia toka Septemba 2005, ambapo walicheza mechi 22 na kufungwa 19 na kutoka sare michezo mitatu.

Sasa Man City wanapeleka matumaini yao kwa klabu ya Leicester City ambao wanapambana na vinara Liverpool leo Jumatano usiku. Iwapo Liverpool watashinda mchezo wa leo, basi watatanua pengo la uongozi wa EPL kwa alama saba.

Upande wa pili kwa mashabiki wa Liverpool matokeo ya City wameyapokea kwa furaha isiyo kifani.

Mashabiki hao kwa kutumia mitandao ya kijamii wamemwagia sifa kocha wa Newcastle Rafael Benitez, na kusema moyoni, yeye bado ni mwenzao.

Benitez amewahi kukinoa kikosi cha Liverpool na ni moja ya wakufunzi wenye historia nzuri kwa kuiwezesha timu hiyo kuchukua Kombe la Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2005.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Rafa Benitez ni kipenzi cha mashabiki wa Liverpool baada ya kuingoza timu hiyo kunyanyua Kombe la Klaabu Bingwa Ulaya 2005
Man United nusura wafungwe
Manchester United chini ya kucha wao wa muda Ole Gunnar Solskjaer nusura wakumbane na kichapo chao cha kwanza baada ya kushinda mechi nane toka kocha huyo achukue uongozi wa timu.

United walitanguliwa na Burnley kwa goli mbili sifuri na kusawazisha katika dakika za lala salama na kuambulia lama moja.

Magoli ya Burnley yalifungwa na Ashley Barnes katika dakika ya 51 na Chris Wood katika dakika ya 81.

Pogba alisawazisha goli la kwanza kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 87 na dakika ya 92 Victor Lindelof aliihakikishia sare United.

Pogba alisawazisha goli la kwanza kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 87 na dakika ya 92 Victor Lindelof aliihakikishia sare United.
"Tumesawazisha kwa njia maridhawa kabisa, wachezaji walikuwa wanaulizwa watafanya nini wakiwa wametanguliwa kwa goli 1-0 ama 2-0 na sasa wametoa majibu kwa njia bora kabisa,"amejitetea Solskjaer.

"Tulimiliki mpira kwa kiasi kikubwa, hatukustahili kufungwa.

"Tumejiangusha wenyewe na tumewaangusha mashabiki wetu hii leo (jana), ila wale waliosubiri mpaka kipyenga cha mwisho wamefurahia matokeo, hivi ndivyo Manchester United ilivyo toka enzi, tunapambana mpaka dakika ya mwisho," amesema Solskjaer.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad