Manara Awajia Juu Wanaopotosha Kuhusu Nyoni

Manara Awajia Juu Wanaopotosha Kuhusu Nyoni
Klabu ya soka ya Simba imeonya watu wanaosambaza taarifa za uongo juu ya majeruhi ya mlinzi wao Erasto Nyoni ambaye aliumia kwenye mchezo wa jana dhidi ya KMKM.

''Kuna taarifa za upotoshwaji zinazoendelea kusambazwa mitandaoni juu ya majeraha aliyoyapata beki wetu Erasto Nyoni kwenye mchezo wa dhidi ya KMKM uliochezwa jana'', imeeleza taarifa ya Simba.

''Ni kweli Erasto anaendelea na vipimo zaidi leo hapa Dar es salaam na taarifa ya ukubwa wa jeraha lake na aina ya tiba atakayopata nitaitoa kesho Saa Saba mchana'', imeendelea kuripoti taarifa hiyo.

Mapema leo zilisambaa taarifa kuwa Nyoni ameumia na atakaa nje ya uwanja kwa miezi miwili mpaka mitatu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad