Maneno ya Babu Tale 'yampa hasira' Fid Q hadi kachukua uamuzi huu


Bila shaka inaikumbuka vita iliyoibuka kati ya Fid Q na meneja wa Diamond, Babu Tale iliyotokea 
mwishoni mwa Novemba mwaka jana. 

Ni baada ya Fid Q kudaiwa kutoa kauli ambayo siyo nzuri kibiashara kwa tamasha la Wasafi Festival. 

Kisha Babu Tale na Mkubwa Fella walisikika wakimponda msanii huyo licha ya kutajwa kama msanii mkubwa wa hip hop Bongo lakini hajawahi kumiliki gari. 

Sasa leo Fid Q ameachia wimbo unaokwenda kwa jina la Mafanikio akimshirikisha Barakah The Prince, rapa huyo ameamua kutumia wimbo huo kujibu maneno ya Babu Tale. 

"Ile kauli ya mafanikio ni kumiliki gari ndio iliyopelekea mimi kuona umuhimu wa kuandika hii 
ngoma ili watu wetu wapate kujua maana halisi ya kunanikiwa," ameeleza Fid Q. 

Licha ya kuandika wimbo huo na kuutoa, utakumbuka Fid Q aliwahi kujibu hilo kwa kuonyesha aina ya gari ambalo analimiliki kwa lengo la kuzima figisu hizo. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad