Mange Kimambi Awashukia Wanaomshauri Mtoto wa Kajala PAULA Kuwa Sio Lazima Kusoma na Kufaulu

Ni vizuri kuona Paula anapata sapoti na wale waliokuwa wanambully mwanzo wameaibika na sasa wako kimya. Ila naona kama sapoti inapitiliza mpaka ushauri unakuwa mbovu.

I’m a very strong believer of education. Sijapenda kabisa wanaompa Paula moyo kwa kumwambia sio lazma elimu na kumpa mifano ya watu waliofanikiwa bila elimu. Jamani naomba tuache kutoa ushauri kama huo kwa mtoto wa kike. Tuache kumpa mifano ya watu walioacha shule wakafanikiwa. Kumbukeni huyu ni mtoto atachagua the easy way out na kumwambia mamake ona mama hata watu wanasema sio lazma shule.

Paula mwanangu shule ni lazima. Hakuna option ingine zaidi ya shule.Nenda shule kachukue degree yako then fanya mambo unayoyataka kama ni biashara au kama ni fashion ila go to school first.

Shule haiongopi hata siku moja. Shule is the best back up plan to have mwanangu.Ni wachache waliacha shule na wakafanikiwa hao mabilionea ambao unaona wanatolewa mifano ni watu ambao waliacha shule baada ya kuona wana plan kubwa na plan ya mitaji walikuwa nayo.

Mamako hapa nna ka-masters kangu hata Magu akisepa nikisema nirudi bongo I can do anything, naweza ingia kwenye siasa etc shule ninayo ni rahisi kuaminiwa kupewa nafasi flani. Hata hapa marekani leo hii nikisema ntafute kazi ya ofisini sikosi ila nimeamua kuwa full time mom. Kwa kifupi wanangu hawawezi kufa njaa nomatter what. .

Kama wewe hukusoma na umefanikiwa basi ni bahati yako. Je siku siku biashara ikifilisika? Nani atakuajiri na wewe ni la 7? Nyinyi ndo wale mtu anasikia huyu alikuwaga tajiri zamani magari kibao ila siku hizi anapanda daladala. Na hata wale wenye kazi maofisini ila waliishia form 4 au 6 watakwambia hawezi kuprogress kazini sababu hawana elimu kubwa. Hakuna promotion ya maana.

Naomba nikupe mfano hai wa ukombozi wa elimu. Director wa Nimr, Dr. Mwele Malecela alitumbuliwa mwaka juzi  . Leo hii yuko anaishi Geneva, bonge moja la bosi huko WHO. Je angekuwa hajasoma? 

Usiposoma utanyanyasika Paula. Uzuri hautokuokoa. Soma mama, huo uzuri wako ukijumlisha na elimu uwiiiiii mbona watu wakatakaa chini. #EducationIsSexy

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad