Mapya yaibuka, mtoto aliyefungiwa Kabatini miezi 5

Mapya yaibuka, mtoto aliyefungiwa Kabatini miezi 5
Uongozi wa hospitali ya Mkoa wa Dodoma umesema kuwa tayari wamemruhusu, Neema Matimbe (15) ambaye inadaiwa mwanaye wa miezi mitano alifungiwa kabatini na mwajiri wake tangu alipozaliwa, lakini hajapata mtu wa kumchukua hivyo atakaa hospitali wakati uongozi ukiwasiliana na



Idara ya Ustawi wa Jamii ili waishi nae kwa sasa.

Imebainika kuwa mama mzazi wa Neema (15) naye ni mfanyakazi wa ndani kama alivyo mwanaye, hivyo kutokana na sababu hiyo, hospitali hiyo imesema ni vigumu kumruhusu binti huyo kwa sababu ya usalama wake.

Akizungumza na www.eatv.tv  leo Januari 15, mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Ernest Ibenzi amesema mama wa binti huyo yupo lakini naye anafanya kazi za ndani jijini Dodoma, jambo ambalo ni ngumu kwa binti huyo kuruhusiwa kuishi naye.

“Changamoto ya huyu binti, Mama yake mzazi pia anafanya kazi za ndani hapa mjini, kwa hiyo hatuwezi kumruhusu kwenda huko mpaka serikali itakapopata nyumba ya kumweka baada ya kuruhusiwa, bado wapo hapa hospitalini", amesema  Dkt. Ibenzi.

Mwalimu Anitha Kimako anayedaiwa kuwa mwajiri wa binti huyo ambaye anatuhumiwa kumpiga na kumshinikiza kumuweka mwanaye kabatini tangu alipozaliwa, alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Januari 7 na kusomewa shtaka la kushambulia mwili ambalo alilikana na kesi hiyo kuahirishwa hadi Februari 7.

Wakati hayo yakiendelea, kijana anayedaiwa kumpa ujauzito binti huyo na kumkataa, Salum Waziri atafikishwa mahakamani muda wowote kujibu mashtaka ya kumpa mimba mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18.

Bofya link hapo chini kumsikiliza Dkt. Ibenzi.



TOP STORIES

SPORT
“Shughuli ya Lechantre imekwisha”-Manara

SPORT
Ngoma ashindwa kuichezea Azam, Kagame

CURRENT AFFAIRS
Amuua mke mwenza na kumzika shambani

CURRENT AFFAIRS
Mbunge wa CHADEMA, ajiuzulu na kujiunga CCM



MOST POPULAR

SPORT
Yanga waeleza sababu ya Makambo kuondoka

CURRENT AFFAIRS
Sababu za kufutwa mashamba sita ya Mo Dewji

CURRENT AFFAIRS
Rais Magufuli apiga 'stop' nyumba kuvunjwa

CURRENT AFFAIRS
Lissu apigiwa kampeni ya urais

ENTERTAINMENT
Msanii Afrika Kusini atoa siri ya kuimba Kiswahili
ABOUT US
ABOUT USADVERTISEJOBSTERMS & CONDITIONSCONTACT USFREQUENTLY ASKED QUESTIONS
NETWORK
IPP MEDIAEAST AFRICA RADIOITVRADIO ONECAPITAL RADIOLOKOPROMO
© 2019 East Africa Television Limited. All Rights Reserved

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad