Marafiki Sahihi ni Njia Sahihi ya Kupata Kile Unachokihitaji


Miongoni mwa sababu zitakazokusaidia kufika mbali kwa kile ukifanyacho ni pamoja na kuwa na marafiki, na si marafiki tu, bali marafiki sahihi.

Marafiki sahihi ni chanzo kikubwa cha kukufikisha kule unakotaka kwenda endapo utaamua kuwatumia vyema marafiki hao.

Utamjuaje rafiki wa kweli.
Rafiki wa kweli ni yule anayekupa ushauri maridhawa kwa kile ukifanyacho, sifa nyingine ya rafiki wa kweli mara nyingi hatakiwi kuwa mtu wa kukusifia tu kwa kile ukifanyacho, bali anatakiwa kuwa ni mwenye kukukosoa na kukupa maarifa zaidi ya kuboresha hicho ukifanyacho.

Na mara nyingi watalamu wa mambo wanatukumbusha kuwa tunapotafuta marafiki sahihi katika maisha yetu tunatakiwa kuhakikisha kila mmoja wetu anatafuta rafiki ambaye anafanya kitu ambacho kinafanana na huyo rafiki, hii itasaidia kubadilishana uzoefu. Kwa mfano kama wewe ni mkulima wa nyanya basi tafuta rafiki ambaye anafanya kilimo hicho pia.

Mwisho nimalize kwa kusema marafiki wa kweli wana mchango mkubwa sana wa kukupa mawazo mapya kama utaamua kuwatumia vyema. Asante.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad