Marehemu Aliyezikwa Miezi Mitano iliyopita Afukuliwa


Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma imeamuru kufukuliwa kwa mwili wa marehemu Cosmas Msote aliyefariki dunia miezi mitano iliyopita ufanyiwe uchunguzi wa chanzo cha kifo chake kilicholeta sintofahamu na kudaiwa kuwa kimetokana na kipigo huku wengine wakidai kuwa kimetokana na shinikizo la damu kama.

Ofisa upelelezi wa polisi mjini Mpwapwa, Makubura Kati amesema ndugu wa marehemu walileta lalamiko kuwa kifo cha ndugu yao kilitokana na kipigo na alizikwa kabla mwili wake kufanyiwa uchunguzi yaani (postmotum).

Mahakama kupitia Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Mpwapwa, Pascal Mayumba imefikia uamuzi huo baada ya kuwapo na ubishani Kati ya taarifa zilizo andikwa na Mganga wa hospitali ya wilaya ya Mpwapwa juu ya chanzo cha kifo chake kilichotokea Oktoba 5, 2018 ambapo tayari wanamshikilia Emmanuel Sindato kuhusika na kifo cha marehemu huyo.

Mmoja wa watoto wa marehemu Julias Msote amesema kuwa wameamua kufukua mwili wa baba yao baada ya kubaini kuwa kifo chake hakikutokana na shinikizo la damu.


“Mwili wa baba toka wanaufikisha hospitalin walisema ulitokana na kipigo na Fomu ya polisi namba tatu walijaza (PF3) sasa ninashangazwa kuambiwa mzee alifariki kwa presha tatizo ambalo hajawahi kuwa nalo Katika maisha yake yote,”aliongea Julias

Aidha amesema wanasubiri taarifa ya daktari aliyefanya uchunguzi huo na kubaini chanzo cha kifo cha marehemu.

Uchunguzi huo unafanywa na mganga mkuu mfawidhi wa hospital ya wilaya Dkt Hamza Mkingule na bibi Afya wa wilaya bi Merry Mabagwa chini ya uangalizi wa polisi wa kituo kikuu cha wilaya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad