Mshindi huyo wa pili katika uchaguzi wa urais amewasilisha pingamizi katika Mahakama ya Katiba kuyakataa matokeo ya uchaguzi akisema kuwa yaligubikwa na udanganyifu
Fayulu amesema kuwa matokeo ya uchaguzi wa Desemba 30, 2018 yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(CENI) yalikuwa yamepangwa na ametoa wito wa kuhesabiwa upya kwa kura hizo
Amesema kuwa Tshisekedi ameshinda uchaguzi huo kutokana na mpango wa siri uliofikiwa kati yake na Rais anayeondoka madarakani, Joseph Kabila
Muungano wa vyama vya upinzani unaoongozwa na Fayulu unadai kuwa kiongozi wao ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 61
Mahakama ya Katiba ina siku 7 za kuisikiliza rufaa hiyo.