Matokeo Kidato Cha Nne Yamtesa Polisi....Afukuzwa Kibarua Kwa Kushiriki Kuiba Mtihani



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amemfukuza kazi askari wa jeshi la polisi aliyekuwa akihudumu kwenye kituo cha Malinyi, PC Hamisi kwa kuhusika kwenye udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika mwaka uliopita.

 Askari huyo alikuwa mmoja wa maafisa usalama waliokuwa na jukumu la kusimamia mitihani hiyo, wakati mitihani ilipofanyika 2018.

Askari huyo ambaye alitajwa kuwa moja ya watu ambao walipanga njama kuhusu zoezi la ufanyaji wa mitihani katika kituo hicho na kusababisha wasimamizi wa mitihani kukitilia shaka kituo hicho na kuanza kukifanyia uchunguzi.

Januari 24, 2019 Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) lilitangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.29 kutoka asilimia 77.09 mwaka 2017 hadi asilimia 78.38, huku likifuta matokeo ya shule moja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad