Matokeo ya Sonia Yamtoa Machozo Monalisa Atamani Uwepo wa Mzazi Mwenzake

Matokeo ya Sonia Yamtoa Machozo Monalisa Atamani Uwepo wa Baba Sonia
MUIGIZAJI maarufu Bongo, Yvonney Cherry ‘Monalisa’ baada ya mwanaye Sonia George Tyson kufaulu kidato cha nne na kupata daraja la kwanza huku somo la Hesabu akiwa amepata A, ame­jikuta akibubujikwa machozi ya fu­raha na kutamani uwepo wa baba wa Sonia, George Tyson aliyetan­gulia mbele ya haki.



Akizungumza na Ijumaa Wik­ienda, Monalisa alisema kuwa alipopata taarifa hizo alishindwa hata kulala lakini kingine kilichowa­tia huzuni ndani ya furaha hiyo ni baa­da ya kukumbuka kwamba baba yake huyo alikuwa akipenda sana mtoto wake huyo asome sana ili aweze kufika elimu ya juu.



“Siwezi kusema furaha ambayo ninayo kwa mtoto wangu huyo lakini Tyson angekuwepo ange­shuhudia ukuu wa Mungu, kwa sababu alipenda sana Sonia asome tena aongoze kitaifa, ndio kitu alichokuwa akikipenda lakini tunashukuru Mungu kwa kuibuka na daraja la kwanza kwani ni wengi waliotamani lakini wameshindwa kupata, yeye amewe­za,” alisema Monalisa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad