Mawaziri Waliobaki na Vyeo Vyao kwa Miaka 10

Mawaziri waliobaki na vyeo vyao kwa miaka 10
Hivi sasa watu kutoka sehemu mbalimbali Duniani wanaendeleza kampeni ijulikanayo kama '10 Years Challenge' katika mitandao ya kijamii, inayoelezea kumbukumbu zao mbalimbali za miaka 10 iliyopita.

Baadhi ya orodha ya Mawaziri ambao wamweza kuhudumu katika nafasi zao kwenye serikali mbili, ikiwemo Serikali ya Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ya mwaka 2009 akiwa madarakani pamoja na serikali ya Dkt John Pombe Magufuli.

Moja ya mawaziri waliobahatika kuhudumu kwenye nafasi katika utawala wa serikali ya awamu ya nne na ya tano ni Waziri wa sasa wa Utumishi na Utawala bora, Gerorge Mkuchika ambaye katika kipindi cha mwaka 2009 ambapo kulikuwa na jumla ya wizara 25, yeye alihudumu kama Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo.

Mwingine ni Waziri wa Ulinzi wa sasa, Dkt Hussein Mwinyi ambaye katika kipindi cha mwaka 2009 alihudumu kwenye nafasi hiyohiyo ya Waziri kamili wa Ulinzi.

Kiongzi mwingine ambaye amefanikiwa kubakia kwenye uongozi wa serikali mpaka sasa tangu mwaka 2009 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli ambaye katika kipindi hicho alikuwa akihudumu kama waziri mifugo na Uvuvi chini ya serikali ya awamu ya nne.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad