Mbao FC yaifunga Gor Mahia na kuitoa nje ya michuano ya SportPesa miamba hiyo ya soka kutoka Kenya

Mbao FC yaifunga Gor Mahia na kuitoa nje ya michuano ya SportPesa miamba hiyo ya soka kutoka Kenya
Kubwa kwenye mchezo wa soka hivi sasa ni michuano ya SportPesa inayoendelea uwanja wa taifa ambapo katika hali isiyo kuwa ya kawaida bingwa mtetezi timu ya Gor Mahia imeyaaga mashindano hayo baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Mbao FC ya Tanzania.


Katika hali isiyokuwa ya kawaida na wala isiyotarajiwa na wengi mabingwa watetezi Gor Mahia wameyaaga mashindano hayo kwa kutolewa na timu changa ya Mbao FC kupitia mikwaju ya penati.

Katika penati hizo Mbao FC imekosa moja kati ya tano ilizopiga wakati Gor Mahia wakikosa mbili kwenye mikwaju hiyo mitano.

Mpaka dakika 90 zinakamilika timu hizo zilitoka sare ya bao 1 – 1 ghali iliyopelekea kupigwa mikwaju ya penati ili kupata mshindi atakayesonga hatua inayofuata.


Bao la kuongoza la Gor Mahia likifungwa na Denis Oliech kupitia mkwaju wa penati baada ya Amos Charles kuunawa mpira ndani ya 18 katika haraka za kuokoa wakati Mbao FC wakipata goli la kusawazisha kupitia Aboubakar Ngalema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad