Mimba Yangu Hainizuii Kupiga Kazi Kama Kawaida”-Ruby

Mimba Yangu Hainizuii Kupiga Kazi Kama Kawaida”-Ruby
Msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye Hivi sasa anafanya vyema na single yake ya ‘Alele’ Helen George ‘Ruby’ amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na  kwamba ni mjamzito Lakini sio kikwazo kwake kwani anapiga kazi kama kawaida.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Ruby  amefunguka kuwa, kabla hajapata mimba alihisi labda akiipata atashindwa kufanya shughuli zake nyingine, lakini hali imekuwa tofauti kwani anapiga kazi kama kawaida.

Mwanzoni kabla sijapata mimba nilijua nikija kupata, basi sitaweza kufanya chochote, nilidhani labda nitakuwa nachoka sana, lakini namshukuru Mungu hali imekuwa tofauti kwani baada ya kuipata sasa hivi napiga kazi kama kawaida na nitaendelea hadi nitakapojifungua“.

Ruby anategemea kujifungua Mtoto Wake wa kwanza muda wowote kuanzia Hivi sasa ingawa Mpaka leo bado hajamuweka wazi nani baba wa Mtoto wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad