Mimi Mars Kuanza 2019 na EP Kali Akiwa Anatarajiwa Kutua Coke Studio Kwa Mara yake ya Kwanza


Mkali wa “Kodoo”, “Shuga” na “Papara” MIMI MARS Kutoka MDEE MUSIC anatarajiwa kushiriki katika msimu mpya wa Coke Studio Africa 2019, kwa mara yake ya kwanza katika kipengele cha “BIG BREAK” akiwakilisha Tanzania. Mimi atashirikiana na KING SAHA (Kutoka Uganda) na YARED NEGU (Kutoka Ethiopia) na Mtayarishaji wa Muziki kutoka Uganda DADDY ANDRE.

 

Pamoja na hilo, mkali huyu wa sauti kutoka katika kiwanda cha muziki Tanzania “MIMI MARS” ameachia EP (Extended Play) kali inayoitwa “THE ROAD” chini ya MDEE MUSIC ikiwa na nyimbo sita. Hii ni EP ya kwanza toka kwa kinda huyu kwenye muziki wa Bongo flava ambapo ndani ameshirikisha vichwa kama Nikki Wa Pili wa Tanzania na Kagwe Mungai toka Kenya. Utayarishaji wa EP hiyo umesimamiwa na Rash Don, Rachi, Fiz na Dedrey.

 


Mimi akizungumzia mafanikio yake,  “Kujiunga Coke Studio ni ndoto ambayo imekuwa kweli, ni wakati sahihi kwa sababu ni muda mrefu nimekuwa nikifuatilia shoo, nikitarajia kupoke simu ya mwaliko. Bado ni mshangao kwangu lakini nimefarijika sana. Uzoefu unanihamasisha na kunihakikishia kwamba nipo katika njia sahihi.” Aliongeza, “Ilikuwa jambo kubwa sana kufanya kazi na Yared na King Saha. Wote ni wasanii wachangamfu na wanaojituma sana, nimechukua mambo mengi sana kutoka kwao katika kipindi cha kurekodi.”

 

Mimi Mars anatarajiwa kufanya vizuri sana kwa mwaka 2019. Akiendelea na kasi yake hii ya kudondosha kazi nzuri kwenye masikio yetu kama ilivyokuwa mwaka 2018 ambapo ulikuwa mwaka mkubwa kwake kwani alifanikiwa kuachia nyimbo 3 (SITAMANI, PAPARA na KODOO) ambazo zinaendelea kufanya vizuri sana.

 

Nyota yake itaendelea kung’aa zaidi kwani ulimwengu wa muziki utamshuhudia kwenye jumba la Coke Studio Africa 2019hivi karibuni akifanya kazi na wasanii wakali wa Afrika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad