Misaada inalemaza - Rais Maguful


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John pombe Magufuli amesema kuwa wakati mwingine misaada inalemaza hivyo ili nchi iendelee ni lazima tujitegemee. 

Rais Magufuli aliyasema hayo katika hafla ya upokeaji wa ndege Jijini Dar es Salaam, alisema Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kutekeleza kwa vitendo dhana ya msingi wa kujitegemea na kupunguza kutegemea misaada kutoka mataifa ya nje.
"Wakati mwingine misaada inalemaza, hivyo ili nchi iendelee ni lazima tujitegemee na sisi tumeamua kuimarisha Shirika letu la ndege la ATCL, kwa sasa zipo ndege sita na tumepanga kuongeza nyingine mbili ambapo moja aina ya Dreamliner ya pili inategemea kuwasili nchini mwishoni mwa mwaka huu,” alisema Rais Magufuli. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Nchini (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi alisema katika kufikia malengo yaliwekwa na Serikali, ATCL imeendelea kutekeleza kwa kasi kubwa kuimarisha mtandao wa huduma katika Shirika hilo kupitia Mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Shirika hilo (2017/22) uliolenga katika kuliendesha shirika hilo katika kuongeza faida. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad